Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO:Somalia iko hatarini kutumbukia kwenye baa la njaa

mkulima Somalia: Picha ya FAO

FAO:Somalia iko hatarini kutumbukia kwenye baa la njaa

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Kumezuka hali ya wasiwasi juu ya usalama wa chakula nchini Somalia kutokana na nchi hiyo kushuhudia kiwango kidogo cha mvua  na hali ya hewa isiyotabirika mambo yanayotia mashaka kuhusu usalama wa chakula. Joshua Mmali na ripoti kamili.

(Taarifa ya Joshua)

Shirika la kimataifa la chakula la kilimo FAO limesema kuwa kuna wasiwasi wa taifa hilo kukabiliwa na njaa hasa wakati ambapo akiba ndogo ya chakula kilichopatikana msimu uliopita ikianza kupungua, bei za vyakula zikipanda, mvua zikiwa zimechelewa kunyesha na hali ya hewa haitabiriki.

Katika ripoti yake inayotoa taarifa za mapema kuhusiana na hali ya udharura inayoweza kujitokeza, FAO imesema kuwa kuendelea kujitokeza mapigano, kuwepo kwa hali mbaya ya hewa ni baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuifanya Somalia kutumbukia tena kwenye janga la njaa.

Mario Zappacosta,  ni mchumi wa FAO mjini Rome akihusika na mfumo wa utoaji taarifa kuhusu hadhari za chakula na anasema ni vyema usaidizi wa haraka ukapatikana kuondoa hali iliyopo, lakini hata kama mvua zitarejea jambo muhimu ni..

 

(Sauti ya Zappacosta)

 

“Tunatarajia kuwa amani na usalama vitarejea nchini humo ili kuruhusu watu kuendelea vyema na shughuli zao za kila siku za kiuchumi na kuweza kutembea kwa uhuru kutoka eneo moja hadi lingine. Hii pia ina umuhimu mkubwa kwa sekta ya ufugaji kwani wafugaji na mifugo yao waweze kutembea kutoka enoe moja hadi jingine kutafuta malisho na maji.”