Kutoka Burundi hadi Haiti: Kanali Nibaruta azungumzia kazi yake MINUSTAH

29 Mei 2014

Katika kuadhimisha Siku ya Walinda Amani leo Mei 29, walinda amani mbali mbali wamekuwa wakizungumzia majukumu yao na maisha yao katika kutekeleza wajibu huu muhimu wa ulinzi wa amani na kusaidia katika kurejesha utulivu katika nchi nyingi wanakofanya kazi.

Nchini Haiti tunakutana na Kanali Anicet Nibaruta, kutoka Burundi, mwenye umri wa miaka 49, akiwa na uzoefu wa miaka minne katika kikosi cha polisi cha Umoja wa Mataifa.

Kanali Nibaruta alijiunga na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Haiti, MINUSTAH, mnamo Agosti mwaka 2012, ambako sasa anahudumu katika kitengo cha kukagua askari polisi wa taifa la Haiti, kama sehemu ya kusaidia katika harakati za kujenga taasisi za utawala bora. Alipotembelea studio za Redio ya Umoja wa Mataifa ya MINUSTAH FM, mwenzetu hapo Walter Mulondi amemuuliza Kanali Nibaruta, kazi yake hiyo ya ukaguzi inahusu nini kila siku.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter