Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya sintofahamu yaendelea kutawala Libya Qadafhi agoma kuondoka na wimbi la wakimbizi laongezeka

Hali ya sintofahamu yaendelea kutawala Libya Qadafhi agoma kuondoka na wimbi la wakimbizi laongezeka

Kwa zaidi ya wiki mbili sasa hali ya wasiwasi, machafuko na wimbi la wakimbizi ndiyo vinavyotawala nchini Libya.

Maefu ya watu wengi wakiwa raia walioandamana mitaani kupinga utawala wa Rais Al Muammar Qadhafi wamelazimika kufungasha virago kukimbia machafuko hususani kwenye mji mkuu Tripoli na mji wa bandari wa Benghazi.

Pia maelfu ya wahamiaji wengi wakiwa wanatafuta maisha nchini humo kutoka nchi mbalimbali zikiwemo za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara wamejikuta katikati ya tafran hiyo. Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na ya misaada ya kimataifa yako nchini humo na hususani mpakani kwa Libya na Tunisia na Libya na Misri kuwasaidia maelfu kwa maelfu ya watu wanaokimbia machafuko.

Miongoni mwa mashirika hayo ni lile la kimataifa la uhamiaji IOM , la mpango wa chakula duniani WFP, la kuhudumia wakimbizi UNHCR, la watoto UNICEF, la afya WHO na mengine ya kimataifa na yasiyo ya serikali kama ICRC. Ungana na Flora Nducha katika makala hii inayotathimini hali nzima inayoighubika nchi hiyo.

(MAKALA NA FLORA NDUCHA)