Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuliwezesha jamii kufunguka kuhusu ukatili dhidi ya jamii Darfur: Mlinda amani Eva

Polisi wanawake huko Darfur hapa wakitoa mafunzo kwa wanawake kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani karibu na El Fasher, Darfur Kaskazini(Picha:UN /Albert González Farran)

Tuliwezesha jamii kufunguka kuhusu ukatili dhidi ya jamii Darfur: Mlinda amani Eva

Kuelekea siku ya ulinzi wa amani duniani hapo kesho, mmoja wa watanzania aliyehudumu kama mlinzi wa amani huko Darfur, Sudan ameelezea uzoefu wake wa utekelezaji wa jukumu hilo akiwa polisi ambapo amesema waliweza kuvunja mipaka ya ukimya hususan masuala ya ukatili kwa wanawake na wasichana ikiwemo ubakaji.

Eva Stesheni mrakibu msaidizi wa polisi Tanzania ambaye alihudumu Darfur kati ya mwaka 2009 na 2011 ameiambia Idhaa kuwa huko El Salam, awali ilikuwa vigumu kupata taarifa lakini..

(Sauti ya Eva-1)

Eva ambaye sasa ni Mkufunzi katika chuo cha taaluma ya Polisi Tanzania akaelezea vile ambavyo walichukua jukumu la kusindikiza wanawake ili wasikumbwe na zahma.

(Sauti ya Eva-2)

Mahojiano kamili na Eva Stesheni yatapatikana kwenye tovuti yetu.