Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

China yakabidhi majengo ya kulinda wakimbizi wa ndani- Juba-Sudan Kusini.

Wakimbizi wa Sudan Kusini Picha Ya UM /Isaac Billy

China yakabidhi majengo ya kulinda wakimbizi wa ndani- Juba-Sudan Kusini.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), umekabidhiwa na serikali ya China majengo yatakayo tumiwa kama vituo vya ifadhi salama kwa wakimbizi wa ndani kwenye mji mkuu waJuba. Majengo hayo yamejengwa karibu na makao makuu ya UNMISS.

Lengo la msaada huo kutokaChinani kusaidia wakimbizi wa kindani wapate ulinzi bora wakati huu wa mzozo.

Nchi hiyo imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe hivi karibuni.

Balozi wa China nchini Sudan Kusini- Bi Ma Quiang alishiriki na kitia saini cheti cha kukamilishwa kwa kazi hiyo.