Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Swala la Makazi Jumuishi laangaziwa ECOSOC

UN Photo/UNICEF/Marco Dormino
@

Swala la Makazi Jumuishi laangaziwa ECOSOC

Nusu ya wananchi wa bara la Africa wataishi mjini ifikapo mwaka 2035, hii ni changamoto kubwa ya miaka inayokuja, na Baraza la uchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa, ECOSOC, limeanza leo mkutano wa siku tatu kwa kujadiliana jinsi ujenzi endelevu wa mji utaleta maendeleo endelevu. Taarifa kamili na Grace Kaneyia

Ujenzi endelevu wa mji ni fursa ya maendeleo, iwe kiuchumi, kijamii ama kimazingira, wakati takwimu zinaonyesha kuwa ongezeko la watu wanaoishi mjini linaendelea kwa kasi kubwa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkutano huo, amesema:

“ Watu wanakuongezeka mjini, halikadhalika changomoto. Sehemu za miji ziko katikati ya changamoto, fursa na ahadi kubwa. Watu wanahamia mjini kufuatilia ajira na fursa zingine. Lakini bado miji mingi inakabiliana na changomoto, zikiwemo miundombinu mibovu, ukosefu wa ajira na uchafu wa mazingira ”

Amesema aliwahi kutembelea mta wa Kibera, Nairobi, nchini Kenya, akiongeza kwamba tofauti za utajiri alizoshuhudia si sawa wala endelevu.

Rais wa Rwanda Paul Kagame, anashiriki mkutano huo ili azungumzie mfano wa ujenzi wa mji wa Kigali, naye amesema

“Ujenzi wa mji bila mpango unasababisha ongezeko la tofauti. Kwa hiyo, swala si tujenge au tusijenge, swala ni je tunaweza kuongoza huu ujenzi pamoja na raia wetu, ili kuleta faida kubwa kwa wote”