Ban azungumzia Sheria za Kijeshi -Thailand

20 Mei 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amezungumzia juu ya hali inayoendelea kuzorota Nchini Thailand, baada ya Jeshi la nchi hiyo kuweka sheria za Kijeshi kuanzia leo tarehe 20 Mai.

 Bwana Ban, kupitia kwa msemaji wake, ameendelea kuhimiza pande zote ambazo zimekuwa zikizozana kisiasa kwa muda mrefu, wajitahidi kushrikiana katika hali ya kutafuta suluhu mwafaka, kwa kupitia mazungumzo ya maridhiano ili wapate kuelewana.

Katibu Mkuu ameelezea kuwa amani na maendeleo ya Thailand yataboreshwa tu kwa kuheshimu misingi na sera za kidemokrasia, pamoja na udumishaji na uendeleshaji wa mazungumzo kati ya pande zote hizo.

Amewasihii pande zote, ziwe na subira, na zijizuiye kutenda ghasia, na kuheshimu haki za binadamu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud