Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiswahili chapasua anga Marekani; Chuo Kikuu cha Columbia chaandaa warsha kuhusu utamaduni wa lugha hiyo

Kiswahili chapasua anga Marekani; Chuo Kikuu cha Columbia chaandaa warsha kuhusu utamaduni wa lugha hiyo

Chuo kikuu cha Columbia, mjini New York, Marekani ni moja ya vyuo vikuu bora zaidi na kinajulikana kwa masomo yake katika maeneo ya lugha, historia na tamaduni za kiafrika. Hivi karibuni idara ya Kiswahili ya chuo hicho kikuu iliandaa kwa mara ya kwanza warsha kuhusu tafiti mbalimbali zinazohusiana na ukanda wa Afrika ya Mashariki, hasa maeneo ya pwani, waandaaji wakiwa ni wahadhiri Kai Kresse na Abdul Nanji. Priscilla Lecomte alikuwa shuhuda wetu kwenye warsha hiyo na fuatana naye kwenye makala hii kufahamu kilichojiri.