Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua za haraka zichukuliwe kudhibiti matumizi mabaya ya pombe:WHO

picha ya WHO/C. Black

Hatua za haraka zichukuliwe kudhibiti matumizi mabaya ya pombe:WHO

Shirika la afya duniani, WHO limetoa ripoti mpya ya mwaka huu kuhusu pombe na afya inayoonyesha kuwa mwaka 2012 pekee watu Milioni Tatu nukta Tatu walifariki dunia kutokana na matumizi mabaya ya pombe. Taarifa ya Alice Kariuki inafafanua zaidi.

(Taarifa ya Alice)

Takwimu hizo zinamaanisha kuwa kila sekunde Moja mtu mmoja anafariki dunia kutokana na unywaji wa pombe ambapo WHO inasema unywaji pombe siyo tu unasababisha utegemezi kwa pombe bali pia huongeza uwezekano wa mtu kupata magonjwa 200 kama vile ini, numonia, Kifua Kikuu na saratani.

Halikadhalika athari za kijamii ambapo kuna masuala ya vurugu zitokanazo na ulevi pamoja na ukatili.

Dkt. Shekhar Saxena, Mkurugenzi wa WHO idara ya afya ya akili na matumizi mabaya ya madawa anasema kile kinachowatia hofu zaidi.

(Sauti ya Dkt. Saxena)

Dkt, Saxena ametaja pia athari za kiuchumi akitolea mfano Afrika Kusini ambayo amesema mwaka 2009, asilimia kati ya 10 na 12 ya pato la ndani la Taifa lilipotea kutokana na matumizi mabaya ya pombe.

WHO imetaka serikali kuchukua hatua kulinda jamii dhidi ya ulevu wa pombe kwani sasa madhara ya kiafya yanazidi kupanuka, halikadhalika kiuchumi na kijamii.