Video ya muziki inayopigia chepuo kampeni ya LGBT yazinduliwa India

30 Aprili 2014

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imezindua video ya muziki ya aina yake iitwayo WELCOME inayopigia chepuo kampeni ya haki za mashoga, wasagaji na waliobadili jinsia, LGBT.

Video hiyo ikiimbwa na mwanamitindo nyota na Celina Jaitly Jaitly kutoka Bollywood India ni ya dakika Mbili na Nusu na inaonyesha maandalizi ya sherehe ya familia moja baada ya mtoto wao wa kiume kuwaeleza kuwa anakuja na mwenza wa maisha yake.

Maandalizi yanakuwa ni kemkem na hatimaye kijana anawasili na mwenza huyo ambaye ni mwanaume, ambapo awali familia inaonekana kusita lakini baadaye wanatambua kuwa kila mtu amezaliwa huru na sawa na ana haki ya mapendo na hivyo ni vyema kufurahi ili kufanya wengine wafurahi.

Hatua hiyo iliibua furaha katika familia na wote walijumuika katika kucheza dansi kwa pamoja.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter