Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO yatuma madaktari kufuatia ajali ya treni Katanga

MONUSCO yatuma madaktari kufuatia ajali ya treni Katanga

Kufuatia ajali ya treni iliyotokea mkoani Katanga Jamahuri ya kidemokrasi aya Kongo DRC Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifia nchini humo MONUSCO, Martin Kobler ametuma madaktari ili kusaidia katika kuhudumia majeruhi.

Bwana Kobler amesema ujumbe huo uko pamoja na wananchi wakati huu mgumu na kuwatakia ahueni majeruhi huku pia akieleza kusikitishwa kwakena vifo vilivyotokana na ajali hiyo.

Amesema kwamba MONUSCO iko tayari kusaidia mamlaka za serikali katika eneo hilo ili wafanikiwe kuokoa majeruhi.