Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yatoa msaada kunusuru waathiriwa wa machafuko Iraq

WFP yatoa msaada kunusuru waathiriwa wa machafuko Iraq

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP, limeanza kutoa msaada wa dharura wa chakula kwa takribani robo ya milioni ya watu walioathiriwa na mzozo katika jimbo la Al Anbar nchini Iraq.

Msaada huo wa WFP ulioanza mwezi huu unalenga kuzifikia familia 48,000 kwa kipindi cha miezi sita . Kaya hizi zinahusisha wakimbizi wa ndani na walioko katika mazingira hatarishi katika maeneo ambako kuna msomganao mkubwa wa watu kutokana na mzozo.

Taarifa ya WFP inamnukuu Mkuu wa WFP nchini Iraq Jane Pearce akisema kutoa msaada wa dharura kwa watu wa Iraq ambao wameathiriwa zaidi na machafuko ndiyo kipaumbele cha shirika hilo.