Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa kunufaisha wananchi kupitia utalii wazinduliwa Tanzania

Mradi wa kunufaisha wananchi kupitia utalii wazinduliwa Tanzania

Utalii ni sekta muhimu na kubwa  katika uchumi wa taifa la  Tanzania. Katika kuhakikisha kwamba sekta hii na sekta kama ya kilimo zinawanufaisha wananchi mradi mpya kwa ajili ya kuimarisha maisha ya watanzania kupitia utalii umezinduliwa. Mradi huu umafadhiliwa na Uswisi na uzinduzi umefanyika katika hoteli ya Kibo, Arusha nchini humo.

Miongoni mwa waliohudhuria ni Mkurugenzi Mkuu wa kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD, Dokta Mukhisa Kituyi, katika mahojiano maalum na Grace Kaneiya wa idhaa hii ameelezea umuhimu wa makubaliano yaliopelekea uzinduzi huo na walengwa hapa ananza kueleza umuhimu wa makubaliano hayo

(MAHOJIANO)