Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa UNCTAD kuangazia umuhimu wa kuongeza thamani za bidhaa

Mkutano wa UNCTAD kuangazia umuhimu wa kuongeza thamani za bidhaa

Kamati ya biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD imeandaa mkutano wa kimataifa wa bidhaa utakaofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe Saba mwezi ujao huko Geneva, Uswisi.

Maudhui ni kuangalia uongezaji wa thamani wa bidhaa zinazouzwa nje ya nchi hususan na nchi zinazotegemea zaidi biashara ya biadhaa kama vile madini ili kukuza uchumi wao.

UNCTAD inasema ukosefu wa sera thabiti na uwazi unakwamisha matunda ya bidhaa hizo kwa wananchi wa kawaida ikisema kuwa uwazi unazuia rushwa na hatimaye kuongeza uwajibikaji. Yanchun Zhang ni mkuu wa kitengo cha sera kuhusu bidhaa kutoka UNCTAD.

(Sauti ya Yanchun)

Nchi nyingi zinazotegemea bidhaa kwa uchumi wao huziuza nje ya nchi bila kuziongezea thamani ya kutosha. Kwa hivyo kwa nchi hizo ili ziweze kunufaika zaidi na maliasili zao kwa maendeleo yao ni changamoto kubwa na hilola kuongezea thamani ndio tutaangazia kwenye mkutano huo wa siku mbili.”