Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wataka adhabu ya kifo kwa raia Misri ifutwe

Umoja wa Mataifa wataka adhabu ya kifo kwa raia Misri ifutwe

Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa leo limepaza sauti kwa mamlaka nchini Misri likitaka kutenguliwa kwa adhabu ya kifo kwa watu 529 iliyotangazwa wiki iliyopita nchini humo. Joseph Msami na maelezo kamili.

(TAARIFA YA MSAMI)

Kundi hilo la wataalamu limeitaka Misri kutoa kwa watuhumiwa mashtka mapya na ya haki ili kuhakikisha sheria za kimataifa za haki za binadamu zinalindwa.

Wataalmu hao pia wameelezea kusikitishwa kwao kutokana na makosa mblaimbali yaliyofanyika wakati wa mchakato wa kesi hiyo kama vile ukosefu wa wanasheria, watuhumiwa kutokuwepo wakati wa hukumu, pamoja na adhabu ya kifo kwa kundi kubwa la watu.

Wamesema kuwa kuendeshwa kwa kesi katika mazingira hayo kumevunja mkataba wa kimataifa kuhusu haki za raia na kisiasa ambazo Misri iliridhia.