Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wabunge wanawake kutoka Kenya wasema wanataka usawa wa kijinsia katika uongozi

Wabunge wanawake kutoka Kenya wasema wanataka usawa wa kijinsia katika uongozi

Mkutano unaoangazia hali ya mwanamke CSW ukiwa unafikia kilele chake leo mjiniNew York, wanawake wabunge kutokaKenyawamesema moja ya changamoto kubwa ambayo nchiyaoinakabiliwa ni kuongezeka kwa nafasi ya wanawake katika maamuzi kwa kuwashirikisha katika vyombo vya kisiasa pamoja na utamaduni unaokandamiza kundihilo.

Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii wanawake hao wanaowakilisha taasisi ya wanawake wabunge nchiniKenyawameelezea hatua watakazochukua ili kuleta mabadiliko. Ungana na Joseph Msami katika mahojiano hayo.