Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apigia debe kilimo cha kaya kwa maendeleo vijijini

Ban apigia debe kilimo cha kaya kwa maendeleo vijijini

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametoa wito kwa serikali ziwawezeshe wakulima wa kaya kwa kubuni sera zinazoweka mazingira stahiki kwa usawa na maendeleo endelevu vijijin, katika kuendeleza ujumbe wa 2014 ambao umetengazwa kuwa Mwaka wa Kilimo cha Kaya.

Hayo ni katika ujumbe wake kwa kongamano na maonyesho ya kimataifa kuhusu kilimo cha kaya mjini Budapest, Hungary, ambao umetolewa kwa niaba yake na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kilimo na Chakula, FAO José Graziano da Silva.

Bwana Ban amesema kongamano hilo linatoa fursa ya kutambua mchango muhimu unaotolewa na wakulima wadogowadogo, jamii za wavuvi na wafugaji katika maendeleo endelevu na katika kutimiza mkakati wa kutokomeza njaa kupitia kwa mifumo endelevu ya chakula.

Amelipongeza pia kongamano hilo kwa kuangazia sehemu tatu za uendelevu, ambazo ni kiuchumi, kijamii na kimazingira, huku akiongeza kuwa mashamba ya kaya huleta pamoja sehemu zote tatu. Ameongeza kuwa moja ya vitu vinavyohitajika katika kuweka mifumo endelevu ya chakula ni kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na midororo ya kiuchumi.