Mradi wa bidhaa zitokanazo na maziwa zabadili maisha ya Kaya Arusha

26 Februari 2014

Harakati za kutekeleza malengo ya maendeleo ya Milenia zinazidi kushika kasi kila uchao kuhakikisha ukomo wake unapofikia mwaka 2015, malengo yote manane yanakuwa yametekelezwa.

Nchini Tanzania, wadau mbali mbali ikiwemo Uholanzi imeshika kasi kupigia chepuo jitihada hizo, mathalani kutokomeza umaskini kwa kuinua kipato, kuwezesha wanawake kiuchumi na hata elimu kwa watoto kupitia mradi wa kutengeneza bidhaa zitokanazo na maziwa. Kiwanda cha Engitenterrat kilichopo Arusha ni mojawapo ya viwanda vinavyosaidiwa na nchi hiyo na vimeleta mabadiliko yaliyoshuhudiwa na Stella Vuzo wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo alipozungumza na Meneja uzalishaji wa kiwanda hicho Bi.Schola Robert. Kwanza anaanza kwa kueleza alikopata mafunzo.