Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani shambulio nchini Somalia

UM walaani shambulio nchini Somalia

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay amelaani shambulio la leo dhidi ya ofisi za makao makuu ya ofisi za serikali kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu. Taarifa zaidi na Joseph Msami.

(Taarifa ya Joseph)

Hili ni tukio lingine la uhalifu linalodhihirisha kuhaha kwa watekelezaji, amesema Kay katika taarifa yake baada ya kukutana na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud .

Ametuma rambirambi kwa familia za waliouawa kwenye shambulio hilo huku akitaka ahueni ya haraka majeruhi.

Bwana Kay amesema wasomali wamechoshwa na mashambulizi na mauaji na ni wakati wa kufungua ukurasa mpya kwenye historia ya nchi hiyo akisema kuwa huu si wakati wa kurudi nyuma bali kusonga mbele.

Ameshukuru vikosi vya usalama vya Somalia na vile vya Afrika kwa uweledi walioonyesha kufuatia shambulio hilo la leo.

Mkuu huyo wa ofisi ya Umoja wa Mataifa Somalia amesema jamii ya kimataifa inaendelea kujizatiti katika kusaidia na kushuhudia Somalia mpya inaibuka na kuimarisha uthabiti wa taasisi zake.