Ongezeko la mahitaji ya dharura laongeza kiwango cha usafirishaji shehena za usaidizi :UNHCR

20 Februari 2014

Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR linasema kufuatia ongezeko la mahitaji ya dharura ya kibinadamu kwenye maeneo mbali mbali ya mizozo duniani, bohari yake iliyoko Dubai huko Falme za kiarabu limeshuhudia ongezeko dhahiri la operesheni ambapo mwaka jana kiwango cha shehena zilizosafirishwa kiliongezeka kwa asilimia 30 ikilinganishwa na mwaka 2012.

Taarifa ya shirika hilo kwa vyombo vya habari inasema kiwango cha mizigo iliyosafirishwa kutoka borahi hiyo kwa mwaka 2012 na 2013 iliongezeka kwa asilimia 100.

UNHCR inasema kumekuwa na ongezeko la shehena 103 mwaka jana kwa nchi zaidi ya 36 duniani ikilinganishwa na nchi 22 mwaka 2012.

Jumla ya bidhaa zilizobebwa zilikuwa kontena 2059 ambapo mwaka jana pekee nchi kama vile Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ufilipino na Syria zilipokea shehena nyingi kutoka bohari hiyo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter