Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua za kuwawezesha wanawake katika radio zimepigwa, juhudi zaidi zahitajika

Hatua za kuwawezesha wanawake katika radio zimepigwa, juhudi zaidi zahitajika

Mwanahabari mkongwe nchini Tanzania Edda Sanga amesema juhudi za kuwainua wanawake katika nafasi ya maamuzi katika vyombo vya habari hususani radio zimezaa matunda jambo linaloweza kusababisha habari chanya ziwahusuzo wanawake.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii Bi Sanga ambaye ni miongoni mwa wanawake wachache waliosikika mwanzoni na kutamba kupitia iliyokuwa Radio Tanzania Dar es salaam sasa TBC Taifa na ambaye kwa sasa ni Meneja wa vyombo vya habari vilivyo chini ya chuo kikuu cha DSM, anasema licha ya mafanikio hayo bado hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa kwani ikilinganishwa na wanaume bado nafasi ya wanawake katika radio ni finyu.

(SAUTI SANGA)

Mahojiano kamili na Bi. Edda yanapatikana kwenye tovuti yetu.