Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na viongozi kadhaa wakati michezo ya Olimpiki ikianza Sochi

Ban akutana na viongozi kadhaa wakati michezo ya Olimpiki ikianza Sochi

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Mashindano ya michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi yanang’oa nanga huko Sochi Urusi jioni ya leo, yakihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon. Wakati wa kuanza michezo hiyo, ujumbe wa video wa Katibu Mkuu utaonyeshwa kwenye sherehe ya ufunguzi.

Tayari leo, Bwana Ban amekutana na viongozi kadhaa wanaohudhuria sherehe hiyo, wakiwemo Rais Xi Jinping, wa Uchina na Rais Viktor Yanukovich wa Ukraine.

Ban na Yanukovich walijadili kwa kina chanzo cha mzozo na matukio ya hivi karibuni nchini Ukraine, pamoja na jinsi ya kushirikiana zaidi na Umoja wa Mataifa katika siku zijazo.

Katibu Mkuu pia amekutana na Sir Philip Craven, rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki ya Walemavu, IPC, na kusema kuwa michezo ya Olimpiki kwa walemavu ni sehemu muhimu ya kuendeleza mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wenye ulemavu.