Baraza la Usalama lahitimisha ziara yake nchini Mali
Uwanja wa ndege wa Bamako nchini Mali, ndege ya Umoja wa Mataifa iliyobeba wajumbe wa Baraza la Usalama ikiwasili tayari kwa ziara maalum nchini humo. …..
Mwenyeji hapa ni Bert Koenders, mwakilishi maalum kwa Katibu Mkuu wa UM nchini Mali na mjumbe mmoja baada ya mwingine anatambulishwa kwa viongozi wa serikali na wale wa Umoja wa Mataifa....
Kutoka uwanja wa ndege ziara inaanza, na lengo ni kujionea hali halisi baada ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyosababisha vifo, majeruhi na maelfu kupoteza makazi. Ziara inafanyika wakati Mali ikiwa tayari imeanza kutekeleza azimio la Ouagdougou lililotaka uchaguzi kufanyika, kuundw kwa taasisi za kibunge na sasa lililobakia ni mazungumzo na vikundi vyenye silaha ili kuleta amani ya kudumu…. Zahabi Oul Sidi Mohamed, Waziri wa Mambo ya nje wa Mali..
Ni kwamba hatuna nia yoyote ya kumuengua yeyote yule anayepaswa kuwemo kwenye mashauriano. Tunataka yawe jumuishi na iwe jumuishi ya dhati! Yaani kujumuisha vikundi vyenye silaha, jumuiya za kiraia na wananchi wote wa Mali ndani ya utofauti wa wa kikabila na kidini.”
Ziara iliwakutanisha na viongozi waandamizi akiwemo Rais .Keita, mawaziri, vikudni vyenye silaha, viongozi wa kiraia, ujumbe ni na hata walitembelea ofisi za MINUSMA huko Mopti na hospitali inayoendeshwa na walinda amani kutoka Togo na kushuhudia mmoja wa askari majeruhi kutoka Chad aliyejeruhiwa karibuni…
MINUSMA ilieleza changamoto ya usalama hususan eneo la kaskazini ambapo ombwe la ulinzi kutokana na kikosi cha Ufaransa kuachia jukumu hilo kwa MINUSMA. Mwishoni mwa ziara, wajumbe wakatoa taarifa yao kuhusu hitimisho la ziara yao wakisema kuna matumaini ijapokuwa mchakato wa amani unasonga taratibu. Hata hivyo wametiwa moyo na suala kwamba pande zote ziko tayari kusonga mbele. Balozi Gerard Araud, mmoja wa wajumbe wa baraza hilo..
(Sauti ya Balozi Araud)
Jambo muhimu zaidi, kwanza Rais wa Jamhuri kwa kauli thabiti amesisitiza kujitolea kuleta Umoja na maridhiano kwa wananchi wa Malli na hilo halikunishangaza sana. Napia upande wa vikundi vyenye silaha vyote vimesema kuwa viko tayari kuhakikisha kuna Umoja na Utaifa wa Mali na vyote vimesema wako tayari kwa mashauriano.”