Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto zaidi ya 20,000 wataanza masomo CAR:UNICEF

Watoto zaidi ya 20,000 wataanza masomo CAR:UNICEF

Watoto zaidi ya 20,000 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wataanza masomo katika madarasa ya muda baada ya machafuko kuwalazimu kuzikimbia nyumba zao na shule zao kufungwa.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wakati shule zote katika mji mkuu Bangui zimefungwa tangu mapema Desemba mwaka 2013, shirika hilo na washirika wake wanaandaa madarasa ya muda ya kusomea katika maeneo yenye wakimbizi wa ndani mjini Bangui, na tayari madarasa 40 ya muda yanafanya kazi. Patrick McCormick ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA PATRICK McCORMICK)

"Wakati kama huu ambapo shule nyingi ziliharibiwa, watoto wanahitaji kupata mazingira tulivu maishani mwao na shule ni njia moja wapo ya kuwatuliza kwa hiyo tumelipa suala la elimu kipaumbele na tutafanya hayo kadri inavyohitajika kabla ya kuanza ushirikiano na serikali ili kuanzisha shughuli upya katika shule za awali."