Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna mpango bado wa usalama wa utoaji wa misaada ya kibinadamu Homs:OCHA

Hakuna mpango bado wa usalama wa utoaji wa misaada ya kibinadamu Homs:OCHA

Msafara wa kupeleka misaada ya kibinadamu kwa raia waliokwama kwenye mji uliozingirwa wa Homs nchini Syria hautaendelea na azma yake hadi utakapohakikishiwa usalama na serikali na makundi ya upinzani imesema ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu na huduma za dharura OCHA. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

OCHA inasema majadiliano baina ya pande hizo mbili zinazokinzana kuhusu fursa ya kuruhusu misaada ya kibinadamu mjiniHomshajazaa matunda yoyote hadi sasa.

Msafara wa misaada umebeba huduma zinazohitajika haraka za chakula, madawa, chanjo na vifaa vingine visivyo chakula ambavyo ni vya kusaidia watu wapatao 2500. Yens Laerke  ni msemaji wa OCHA mjiniGeneva.

(SAUTI YA JENS LAERKE)

“Majadiliano baiana ya wapinzani wenye silaha na serikali yanaendelea kwa mtazamo wa kutoa fursa ya misaada kuingi mjini Homs na pia kuruhusu raia kuhamishwa . Na itakuwa ni juu ya pande hizo mbili makundi ya wapinzani na serikali , kujadiliana miongoni mwao ili kutuwezesha kuweka mazingira na hali ambayo tutaweza kutoa msaada kwa njia ambayo ni salama kwa wanaopeleka misaada hiyo na wanaoipokea.Kuna mashirika mengi ambayo yako tayari kupeleka msaada kwa watu hadi 2500. Idadi ya malori , idadi ya msaada utaopelekwa na njia itakayotumika kufikisha  ni sehemu ya mjadala baiana ya serikali na makundi ya upinzani.”

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema limeongeza operesheni zake ili kuweza kulisha watu milioni 4.25 mwezi huu , lakini kufungwa kwa barabara kunasitisha usafirishaji wa chakula nchi nzima.