Ban azungumza na rais wa Ukraine kwa simu leo

27 Januari 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza kwa njia ya simu na rais wa Ukraine . Viktor Yanukovych ambapo viongozi hao wamejadili hali nchini humo.

Katika mazungumzo hayo Bwana Ban amemfahamisha rais wa Ukraine kwamba amekuwa anafuatilia kwa karibu hali livyo nchini humo na kumueleza kuhusu hatua zilizopigwa hivi karibuni nchini humo.

Katibu Mkuu pia amerejelea tamko lake la January 20 alilotaka majadiliano jumuishi na endelevu kwa pande zote ili kutafuta suluhu la mzozo na kuzuia umwagaji damu. Amemtaka Rais Yanukovych kuongoza katika njia ya ujenzi wa majadiliano ili kusaidia kutanzua mgogoro katika nchi yake kwa njia ya amani na maafikiano.

Bwana Ban amemuhakikishai kiongzi huyo kuwa Umoja wa Mataifa uko na taifa la Ukarine na watu wake daima.