Baraza la Usalama laelezwa kuhusu ubakaji na hatari ya mauaji ya kimbari CAR

22 Januari 2014

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari, Adama Dieng, ameliambia Baraza la Usalama leo kuwa licha juhudi zilizofanywa na viongozi wa kidini kama kasisi na Imam wa mji wa Bangui kuendeleza amani na mazungumzo, ni mafanikio machache sana yaliyopatikana.

Akilihutubia Baraza hilo ambalo limekutana kujadili hali nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bwana Dieng amesema kuna haja ya dharura ya kuunga mkono vikosi vya ujumbe wa Muungano wa Afrika, MISCA, na juhudi za kuendeleza mazungumzo ya amani na maridhiano ya kitaifa. Ameongeza kuwa kuna haja ya kuendeleza mazungumzo baina ya Wakristo na Waislamu kama njia ya kuondoa chuki na migawanyo iliyopo nchini humo sasa

“Machafuko yalodhaniwa awali kama vurugu kati ya waasi wa zamani wa Seleka na wanamgambo wanaowapinga, haraka yaligeuzwa kuwa vurugu hatari sana kati ya Waislamu na Wakristo, na kiwango cha chuki kati ya jamii hizi, kilinishangaza. Uchochezi wa kutenda ukatili kwa misingi ya dini au kabila, na mashambulizi ya kukusudia dhidi ya raia kwa kutokana na imani au kabila, ni ishara za hatari ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya kimbari.”

Naye Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika maeneo ya vita, Zainab Hawa Bangura, amesema hali nchini CAR imezidi kuzorota, na ukatili wa kingono umeendelea kuenea katika machafuko hayo.

“Kati ya Januari na Novemba mwaka 2013, Umoja wa Mataifa ulirekodi yapata visa 4,530 vya ukatili wa kingono, ulotekelezwa na wanaume wenye silaha, ambao wanaaminika kuwa waasi wa zamani wa Seleka mjini Bangui, Bwali, Busembela, Damara, Baki, Sibut na Prefecta de  Luhambede. Na kuna ripoti kuwa ukatili wa kingono katika vita umeendelea kutumika.”

Amesema kuna pia ripoti kuwa ndoa za lazima kwa watoto pia zimefanywa katika mzozo huo.