Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Michezo yaweza kukuza ajira kwa vijana: ILO

Michezo yaweza kukuza ajira kwa vijana: ILO

Shirika la kazi duniani, ILO, linasema waajiri walio wengi hukwepa kuwaajri vijana wengi  kwa  kigezo cha ukosefu wa  ujuzi wa kazi huku wengi wakiwa hawazingatii kwamba vijana wanaweza kupata ajira iwapo waajiri watazingatia ujuzi wao katika michezo.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa ajira za vijana wa ILO kanda ya Asia na Pacific Matthieu Cognac ujuzi katika ajira mathalani nidhamu, ubunifu, kuzingatia muda na mengineyo ni mambo ambayo yanaweza kufundishwa wakati wa mafunzo ndani ya kazi na kwamba kwa kuelewa jinsi gani ujuzi kama maadili na mawasiliano unavyoweza kuendelezwa kupitia michezo ni njia muafaka ya kukuza ajira kwa vijana.