Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa waelekeza juhudi Somalia kuimarisha usalama na ujenzi wa taifa

Umoja wa Mataifa waelekeza juhudi Somalia kuimarisha usalama na ujenzi wa taifa

Somalia, baada ya miongo miwili ya vita nchini humo juhudi za Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa katika kusaidia ujenzi wa amani ya kudumu zimekuwa dhahiri ikiwemo kuhakikisha ratiba ya kuwa na serikali ya shirikisho na uchaguzi mwaka 2016 inazingatiwa, na  usaidizi wa vikosi vya Afrika nchini humo AMISOM. Yote yameendelewa kuzingatiwa ikiwemo AMISOM ambapo muda umeongezwa halikadhalika idadi ya askari. Nicholas Kay ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa UM nchiniSomalia.

 (Sauti ya Balozi Kay)

"Nalishukuru baraza kwa usaidizi wao usiotetereka kwa kazi yetu Somalia. Itoshe kusema kuwa sote tuko katika maandalizi ya maisha bora. Somalia mpya inayoibuka inahitaji kuungwa mkono na sisi. Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono sauti za matumaini na si za kukata tamaa, fursa na siyo mizozo."

Balozi Augustine Mahiga wakati akikabidhi kijiti kwa balozi Kay  aliangalia mbali zaidi mustakhbali wa Somalia...

(Sauti ya Mahiga)