UNICEF yataka watoto Sudan Kusini wapatiwe ulinzi

23 Disemba 2013

Marafiki wote wa Sudan Kusini walio na matumaini makubwa na taifahilochanga, wana hofu kubwa juu ya kile kinachoendelea nchini humo hivi sasa, amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto,UNICEFAnthonyLake. Taarifa hiyo inakuja wakati hali ya mapigano ikiendelea kuripotiwa nchini humo na wananchi wakiwa wamekimbilia kusaka hifadhi kwenye vituo vya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini.BwanaLakeamesema UNICEF inatumai kuwa wahusika wa ghasia hizo na wale wenye ushawishi watachukua kila hatua kulinda watoto pamoja na kusitisha mapigano. Amesema watoto hawawajibiki na vurugu zozote na hata kile kilichosababisha zitokee. Badala yake amesema watoto ni kizazi ambacho kinaweza kufikia matumaini na ustawi ambamo kwao taifahilolilianzishwa ili liweze kutimiza. Kwa mantiki hiyo ametaka watoto hao wapatiwe ulinzi kwa mustakhbali wa taifahilo.