Biashara baina ya nchi zinazoendelea yaongezeka: UNCTAD

17 Disemba 2013

Biashara ya bidhaa nchi za nje imeongezeka mara tatu duniani katika miongo miwili iliyopita na kufikia zaidi ya dola Bilioni 18 huku asilimia 25 ya kiwango hicho kikitoka nchi za kusini au zinazoendelea. Hiyo ni kwa mujibu wa kijarida cha takwimu kutoka kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa kilichotolewa leo.

Kijarida hicho kimesema biashara ya nje kwa nchi hizo hata hivyo inaongozwa zaidi na nchi za Asia ikifuatiwa na zile zaAmericaya Kusini, ingawa biashara baina ya nchi za Afrika inaonekana kushamiri katika kipindi hicho cha kuanzia mwaka 1995.

UNCTAD inasema nchi za Afrika zimenufaika kwa kiasi kikubwa na mabadilishano ya biashara na nchi zaAsia. Mathalani mwaka jana pekee, thamani ya biashara yaChinakwa bara la Afrika ilikuwa dola Milioni 970. Misri imetajwa kuwa miongoni mwa nchi zilizonufaika na kupanuka kwa biashara kati yaAsiana Afrika. Bidhaa zinazohusika kando mwa mafuta na gesi ni vifaa vya umeme na elektroniki.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud