Ban azungumzia umuhimu wa wanawawake, asasi za kiraia katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi .

3 Disemba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumzia umuhimu wa asasi za kiraia , viongozi wa kijamii na wanawake katika kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Katika mkutano na waziri wa mazingira wa Peru Manuel Pulgar-Vidal, katibu mkuu ambaye anahitimisha ziara yake nchini humo amesema anajivunia namna wanawake na asasi za kiraia nchini humo zilivyoonyesha ubunifu katika utekelezaji wa utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na kupanda miti.

Bwan Ban amesema wakati Peru inatarajiwa kuwa mwenyeji wa kongamano la kimataifa la mabadiliko ya tabia nchi mwakani, anatumaini kwamba nchi hiyo itachangia pakubwa katika kuidhinishwa kwa mkataba wa kimataifa kuhusu mwabadiliko ya tabia nchi mwak 2015.