Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kila mtu atanufaika tukijumuisha walemavu kwenye ajira: ILO

Kila mtu atanufaika tukijumuisha walemavu kwenye ajira: ILO

Hali ya wanawake na wanaume walemavu kwenye soko la ajira linatia hofu na mashaka makubwa kwani wana fursa ndogo zaidi ya kuajiriwa kuliko wasio walemavu na hata wakiajiriwa wengi wao huwekwa katika sekta ambazo malipo yake ni haba.

Amesema Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kazi duniani, ILO Guy Rider katika kuadhimisha siku ya walemavu hii leo. Bwana Ryder amesema ajira jumuishi bila kujali mwonekano wa mtu itatoa manufaa kwa jamii nzima hivyo amesema…

 (Sauti ya Ryder)

“Tunatakiwa kuondoa vikwazo na kufungua milango kwa jamii jumuishi. Milango ya ujasiriamali na sehemu ya kazi inapaswa kufunguliwa kwao pia.”