Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upungufu wa wafanyakazi sekta ya afya ni dhahiri, tumechukua hatua:Tanzania

Upungufu wa wafanyakazi sekta ya afya ni dhahiri, tumechukua hatua:Tanzania

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani WHO inasema dunia itakuwa na upungufu wa wafanyakazi milioni 12.9 katika sekta ya afya ifikapo mwaka 2035, huku kwa sasa  upungufu huo ni milioni 7.2, . Serikali yaTanzaniainakiri upungufu huo kuikabili sekta ya afya na kuelezea mikakati iliyopo katika kukabilina na upungufu wa wafanya kazi wa sekta ya afya kwa kuongeza vyuo vya udaktari na kuendesha sekta hiyo kibishara.

Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa naibu waziri wa afya wa Tanzania Dk Seif Rashid anasema mikakati hiyo inakabiliana na ongezeko la magonjwa na ajali lakini kwanza anaanza kuainisha mikakati ya kielimu.

 (Sauti Dk Rashid-Mahojiano)