Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kusaidia serikali y Ufilipino baada ya kimbunga Haiyan

WFP kusaidia serikali y Ufilipino baada ya kimbunga Haiyan

Shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema linaimarisha operesheni zake nchini Ufilipino , na kupeleka msaada wa dharura kuisaidia serikali kutoa msaada kwa walioathirika na kimbunga Haiyan au Yolanda kama kinavyojulikana katika nchi hiyo. Maafisa wa WFP wameungana na timu ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Ufilipino ili kutathimini uharibifu kwenye jimbo la Leyte na Samarna timu nyingine inatarajiwa kuwasili punde. WFP inakusanya akiba ya chakula katika vituo vyake vyote duniani.

WFP imesema imeshakusanya dola milioni 2 kwa ajili ya kusaidia lakini itaomba fedha zaidi kutokana na mahitaji yatakavyozidi kubainika.  Limeongeza kuwa tani 40 za biskuti zenye kutia nguvu zinatarajiwa kuwasili nchini humo kutoka Dubai hivi karibuni huku shirika hilo likitafuta chakula kingine kuhakikisha mahitaji ya lishe yanapatikana haraka.