Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na athari za kimbunga Haiyan Ufilipino:

Ban asikitishwa na athari za kimbunga Haiyan Ufilipino:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amestushwa na kusikitishwa na athari kubwa zilizosababishwa na kimbunga Haiyan au Yolanda ambapo watu wengi wamepoteza maisha na miundombinu kuharibiwa vibaya. Ban ametuma salamu za rambirambi kwa watu na serikali ya Ufilipino hususani kwa waliopoteza ndugu na jamaa, nyumba zao au kuathirika kwa aina yoyote na kimbunga hicho. Ban amewahahakikishia watu wa Ufilipino kwamba mashirika ya Umoja wa matyaifa ya misaada na wadau wengine wanafanya kazi kwa karibu na serikali ili kusaidia juhudi za misaada na kutathimini hali halisi ili kuhakikisha misaada ya muhimu inapelekwa haraka.