Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP yakaribisha hatua ya Marekani kuridhia mkataba kuhusu zebaki:

UNEP yakaribisha hatua ya Marekani kuridhia mkataba kuhusu zebaki:

Marekani imepiga jeki juhudi za kimataifa za kupunguza gesi chafuzi itokanayo na metali nzito baada ya kuridhia mkataba wa Minamata kuhusu zebaki. Mkataba huo uliopitishwa tarehe 10 Oktoba nchini Japan na kupewa jina la mji ambao maelfu ya watu walidhurika na sumu ya zebaki katikati ya karne ya 20 sasa umetiwa saini na nchi 93. Flora Nducha wa Idhaa hii amezungumza na afisa wa habari wa UNEP Njoroge Waiganjo. Ameanza kwa kumuuliza umuhimu wa nchi kuridhia mkataba wa Minamata:

(SAUTI YA NJOROGE)