Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabilioni ya dola yaahidiwa kwa ajili ya ukanda wa Sahel

Mabilioni ya dola yaahidiwa kwa ajili ya ukanda wa Sahel

Benki ya dunia imeahidi dola Bilioni 1.5 ilhali Umoja wa Ulaya umeahidi dola bilioni 6.75 kwa ajili ya kusaidia maendeleo kwenye nchi Sita zilizo Ukanda wa Sahel barani Afrika kwa kipindi cha miaka Saba. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(TAARIFA YA JASON)

Tangazo hilo linajiri wakati kunapofanyika ziara ya kihistoria kwenda eneo la Sahel ziara inayofanywa na viongozi wa maendeleo wakiongozwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kujadili masuala yanayohusu amani na usalama wakiwemo  viongozi wa Mali, Niger , Burkina Faso na Chad.

Kati ya wanaotarajiwa kushuhudia shughuli hiyo ni pamoja na rais wa Benki ya dunia Jim Yong Kim , kamishina anayehusika na maendeleo kutoka kwa Jumuiya ya Ulaya Andris Piebalgs , mwenyekiti wa Muungano wa Afrika Nkosazana Dlamini Zuma na rais wa benki ya Afrika Donald  Kaberuka.

Benki ya dunia imetoa ahadi ya miaka miwili ambapo itafadhili masuala ya kuzisaidia jamii kukabiliana na athari zinazotokana na majanga ya kiasili, kuboresha miundo mbinu na kuhakikisha kuwepo fursa sehemu za vijijini.