Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafanikio dhidi ya Kifua Kikuu hatarini kutoweka: WHO

Mafanikio dhidi ya Kifua Kikuu hatarini kutoweka: WHO

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani, WHO inaonya kuwa mafanikio yaliyopatikana katika kukabiliana na ugonjwa wa Kifua Kikuu yako hatarini kutoweka. Ripoti hiyo inayotokana na taarifa kutoka mataifa 197 na maeneo inataja mambo mawili yanayotia hatarini mafanikio ya tiba iliyookoa maisha ya zaidi ya watu Milioni 22 duniani kote. Mosi ni wagonjwa Milioni Tatu dunini kote kutofikiwa na mfumo wa afya wa kitaifa na hivyo penginepo kushindwa kupata tiba na piil ni janga la kifua kikuu sugu, MDR-TB ambapo WHO inasema kuwa uwezo wa kuwapima na kuwatibu wenye kifua kikuu sugu hautoshelezi. Mkurugenzi wa WHO anayesimamia mpango wa TB duniani, Dokta Mario Raviglione amesema mwaka 2012 pekee watu Laki Nne na Nusu waliugua Kifua Kikuu sugu ambapoChina,Indiana Urusi zinaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi. WHO imependekeza mambo matano ya kufanya ikiwemo kuhakikisha mifumo ya afya ya kitaifa inapanuliwa ili kujumuisha tiba dhidi ya Kifua kikuu, janga la kifua kikuu sugu lipatiwe jibu na kulinda mafanikio yaliyopatikana katika kutibu ugonjwa huo.