Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tujenge utamaduni wa kuzuia vifo, majeruhi na magonjwa kazini: ILO

Tujenge utamaduni wa kuzuia vifo, majeruhi na magonjwa kazini: ILO

Shirika la Kazi Duniani(ILO) limesema nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa lazima zifanye kazi kwa bidii kuimarisha usalama na afya katika maeneo ya kazi.

Tamko la ILO linalotaka kupunguzwa kwa vifo kazini, majeruhi na magonjwa duniani linakuja dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya usalama na afya makazini hii leo.

Taarifa ya ILO inamnuku Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Guy Ryder akisema kuwa sababu za kiuchumi au msukumo wa kupata faida hauwezi kuachiwa uruhusu kupindisha utaratibu.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mazingira hatarishi ya kazi yanasalia tishio la kila siku kwa mamilioni ya wafanyakazi duniani ambapo zaidi ya wafanyakazi milioni 300 wanakabiliwa na majeraha katika kazi zisizo hatarishi , zaidi ya 800,000 wakijeruhiwa kila siku kazini wakati zaidi ya watu 6,000 hufa kutokana na ajali na magonjwa kazini idadi inayofikia milioni 2.3 ya vifo kila mwaka.

Mkuu huyo wa ILO amesema kila mmoja anaweza kushiriki kuzuia vifo kazini, majeraha na ugonjwa kwa kujenga utamaduni huo.