Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujuzi ndio nguzo kuu ya kuwepo uchumi usioathiri mazingira nchini Ushelisheli: UM

Ujuzi ndio nguzo kuu ya kuwepo uchumi usioathiri mazingira nchini Ushelisheli: UM

Kuibuka kwa mahitaji ya kutaka kuwepo kwa harakati za uchumi ambazo zinajali mazingira, inamaana kuwa kuwepo utaalamu ndiyo inastahili kuwa ajenda kuu  kwenye mfumo wa elimu nchini Ushelisheli kwa mujibu wa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki ya kupata elimu Kishore Singh.   Amesema elimu ya kiufundi na ushirikiano na viwanda na biashara ni lazima uboreshwe kuhakikisha kuwa Ushelisheli imepata utaalamu unaohitajika katika ujenzi wa taifa. Mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa amekubaliana na hatua zilizopigwa hivi karibuni  katika sekta ya elimu na serikali ya Ushelisheli lakini hata hivyo akaonya kuwa hatua zilizopigwa zinaweza kuwa kwenye hatari ikiwa shughuli ya kuwaajiri walimu na kuwapa mafunzo hazitifanywa kwa haraka. Bwana Singh amesema kuwa upungufu wa walimu walio na ujuzi ni tatizo kubwa kwa kuwa taaluma hiyo haivutii wengi akiongeza kuwa ikiwa viwango vya elimu vitahitaji kuboreshwa hatua ni lazima zichukuliwe.

Akiwa ziarani nchini Ushelisheli mjumbe huyo maalum alikutana na rais James Michel na maafisa wengine wa ngazi za juu serikalini pamoja na waakilishi wa mashirika ya umma pamoja na mashirika yasiyokuwa ya serikali.