Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Kimataifa ya wanawake wa vijijini yaangaziwa

Siku ya Kimataifa ya wanawake wa vijijini yaangaziwa

Kwa mara ya kwamnza siku ya wanawake wa vijijini iliadhimishwa Oktoba 15 mwaka 2008. Siku hii iliyoanzishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika azimio 62/136 la tarehe 18 Desemba mwaka 2007 linatambua jukumu na mchango wa wanawake wa vijijini pamoja na wanawake wa makabila ya asili katika kukuza kilimo na maendeleo vijijini ikiwemo kuimarisha usalama wa chakula na kupunguza umaskini katika maeneo hayo.