Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhusiano baina ya Sudan na Sudan Kusini wajadiliwa:

Uhusiano baina ya Sudan na Sudan Kusini wajadiliwa:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na waziri wa mambo ya nje wa Sudan Ali Ahmed Kartiwamekutana na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo uhusiano baina ya Sudan na Sudan Kusini, hali ya Darfur, Abyei, Kordofan Kusini na jimbo la Blue Nile

Ban amekaribisha matokeo ya mikutano mitatu ya mwezi septemba baina ya Rais Al-Bashir wa Sudan na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini. Lakini pia ameelezea hofu yake kuhusu kuendelea kwa mvutano kwenye jimbo la Abyei, vita vya Darfur na mapigano yanayoendelea jimbo la Kordofan Kusini na Blue Nile.

Amesisitiza haja ya kuhakikisha kuna fursa ya kufikisha misaada ya kibinadamu na uhuru wa mpango wa UNAMID kuingia katika maeneo hayo.Katibu ameitaka serikali ya Sudan kuwa na mazungumzo yatakayohusisha makundi yote ya upinzani ili kushughulikia chanzo cha vita Sudan