Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Myanmar ichunguze mapigano kati ya jeshi dhidi ya waislamu

Serikali ya Myanmar ichunguze mapigano kati ya jeshi dhidi ya waislamu

Mtalaam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu huko Myanmar, Tomás Ojea Quintana ameitaka serikali ya nchi hiyo kuchunguza ripoti za mapigano makali kati ya vikosi vya serikali na waumini wa kibuda na kiislamu kwenye jimbo la Rakhine.

Mapigano hayo yaliyotokea kwa kipindi cha miezi 18 iliyopita yamedaiwa kusababisha zaidi ya watu Laki Moja na Elfu Kumi kukimbia makwao.

Mtaalamu huyo amesema amepata ripoti kuwa waislamu wa Rohingya wameuawa au wamejeruhiwa, halikadhalika afisa mmoja wa usalama wakati wa operesheni huko Maungdaw,  huku wanawake na watoto wakikamatwa kufuatia mapigano hayo.

Quintana amesema iwapo kulikuwepo vifo au majeruhi, serikali yaMyanmarinapaswa kuchunguza  haraka kwa mujibu wa sheria za kimataifa na kuwawajibisha wahusika. Katika taarifa yake amesema hatua hiyo inaweza kuzuia kutokea kwa ghasia zaidi.

Katika taarifa yake ya hivi karibuni kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bwana Quintana aliseam kuwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu hukoMyanmarunatishia mchakato wa marekebisho ya kidemokrasia na maridhiano ya kitaifa.