Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UM azungumzia hatua za ushirikiano wa kimataifa kwa maendeleo:

Mkuu wa UM azungumzia hatua za ushirikiano wa kimataifa kwa maendeleo:

Kumekuwa na hatua kubwa katika kufikia lengo la ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ambalo ni lengo nambari 8 la milenia kati ya malengo yaliyoafikiwa na viongozi wa dunia mwaka 2000 kutokomeza umasikini. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon wakati wa uzinduzi wa ripoti ya mwaka 2013 ya kitengo maalumu cha kufuatilia mapengo ya kufikia malengo ya maendeleo ya milenia

Ban amewakumbusha waandishi wa habari kwamba alianzisha kitengo hicho mwaka 2007 kufuatilia hatua za jumuiya ya kimataifa katika kuhakikisha na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

“ Leo hii ninafuraha kuripoti hatua kuhusu lengo namba 8, ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo. Kama ripoti inavyoonyesha ushuru katika usafirishaji nje kutoka mataifa yanayoendelea umeshuka. Usafirishaji kutoka nchi zinazoendelea kwenda kwa zilizoendelea umepanda, huku kiwango kikubwa cha usafirishaji kutoka nchi masikini unaruhusiwa bila kodi yoyote. Na fursa ya teknolojia ya simu za mkononi na internet inaendelea kupanuka”

Ban amesema baadhi ya madawa kama ya kufumbaza virusi vya HIV/ na ukimwi yanaanza kupatikana kwa gharama nafuu, hata hivyo ameongeza kuwa bado kuna kazi inahitajika kutimiza kabisa malengo yote.