Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa nne wa kiarabu wa kuboresha ushirikiano wa kibinadamu wango’a nanga Kuwait

Mkutano wa nne wa kiarabu wa kuboresha ushirikiano wa kibinadamu wango’a nanga Kuwait

Chini ya uongozi wake naibu waziri mkuu ambaye pia ni waziri wa mambo ya kigeni nchini Kuwait Sheikh Sabah Khaled Al-Hamad Al-Sabah , mkutano wa nne wa kila mwaka kuhusu ushirikiano na kubadilidshana habari kwa huduma bora za kibinadamu umeng’oa ngana nchini Kuwait.

Mkutano huo uliondaliwa na shirila la kimataifa la kiislamu linalohusika na ufadhili IICO , likiwemo Shirika la direct Aid pamoja na shirika la kuratibu masualaya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA unawaleta pamoja watu mashuhuri kutoka kwa serikali , sekta za kibinadamu na za kibiashara kujadili changamoto zinazokumba mashirika ya kibinadamu. Mwenyekiti wa bodi ya IICO Abduallah Al Ma’atouq anasema kuwa mkutano huu unalenga kupanua ushirikiano katika masuala ya kibinadamu na kuhakikisha kuwepo viwango vya kimataifa Mkutano huo wa siku tatu utajadili changamoto za kibinadamu zinazoukumba ulimwengu wakati huu na njia za kuhakikisha kuwepo ushirikiano wakati wa dharura. Mkutano huo amabo utakamilika siku ya Alhamisi utaangazia suala la kuwashirikisha vijana katika huduma za kibinadamu.