Wakimbizi 107 wa Syria walio Lebanon kuelekea Ujerumani Jumatano:UNHCR

10 Septemba 2013

Jumla ya wakimbizi 107 raia wa Syria wanatarajiwa kuondoka nchini Lebanon kwa makao ya muda nchini Ujerumani kupitia kwa mapngo uliotangazwa mwezi machi mwaka huu. Kundi hilo la wakimbizi linaelekea mjini Hanoverna ndilo la kwanza kupata msaada wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR.

Wakiwasili nchini ujerumani wakimbizi hao watapelekwa  eneo la Friedland ambapo watakaa kwa muda wa siku 14 wakipata mafuzo  kuhusu utamadunia wa Ujerumani ikiwemo lugha, shule na huduma za afya. Baada ya wiki hizo mbili wakimbizi hao watapelekwa sehemu tofauti nchini Ujerumani ambao watapewa makao kwenye vituo vidogo ambapo pia watapata huduma za afya, elimu na huduma zingine za kijamii. Kwa muda ambao watakaa huko wakimbizi hao watakuwa na haki ya kufanya kazi wakiwa na vibali vya miaka miwili na ruhusu  ya kuongeza muda wao wa kukaa ikiwa hali nchini Syria itasalia ilivyo.