Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Aina za ngano zinazohimili magonjwa kuanza kulimwa Kenya:FAO

Aina za ngano zinazohimili magonjwa kuanza kulimwa Kenya:FAO

 Aina mbili mpya za ngano zinazohimili magonjwa zimeanzishwa kwa wakulima nchiniKenya. Tangazo hilo limetolewa Ijumaa na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO.

FAO inasema imekuwa ikifanya kazi pamoja na shirika la kimataifa la nguvu za atomic  (IAEA) katika kuanzisha aina hizo mpya za ngano. Kwa mujibu wa FAO mashirika hayo yanasimamia ushirikiano wa kikanda wa miradi ya kuanzisha aina mbalimbali za ngano ambazo zinahimili aina Fulani ya fangus ambayo inasababisha mche wa ngano kuoza.

FAO inasema kuoza kwa mche wa ngano ni tatizo lililokuwa limedhibitiwa  kwa zaidi ya miaka 30 hadi pale lilipobainika tena nchini Uganda mwaka 1999 na kusambaa nchi jirani ya Kenya. Imeongeza kuwa ugonjwa huo ambao unaweza kuathiri asilimia 70 hadi 100 ya mavuno ya ngano, umesambaa piaIran,Yemen na Afrika ya Kusini na kutishia mazao hadi maeneo ya mbali kama India.

Kwa mujibu wa FAO kwa siku mbili zilizopita maelfu ya wakulima waKenyawamezuru chuo kikuu cha Eldoret Magharibi mwa Kenya kwa maonyesho ya siku mbili ya kilimo  yanayotanabaisha teknolojia mpya ya kilimo.