Skip to main content

Mataifa yatakiwa kutekeleza muafaka wa Cancun:Figueres

Mataifa yatakiwa kutekeleza muafaka wa Cancun:Figueres

Afisa wa ngazi ya juu katika masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa kwenye Umoja wa Mataifa amezishauri nchi kulitilia maanani suala la kupunguza gesi zinazochafua mazingira.

Pia ametaka kuzisaidia nchi zinazoendelea kupambana na tatizo la kuongezeka kwa joto duniani wakati ambapo mkutano wa Umoja wa Mataifa unapoendelea mjini Bangkok. 

Christiana Figueres amesema kuwa serikali zina nafasi nzuri kwenye mkutano wa Bangkok kutekeleza zilizoyafikia kwenye mkutano wa Cancún na kutafuta njia za kupata mafanikio kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa utakaondaliwa mjini Durban.

Kati ya yaliyoafikiwa kwenye mkutano wa Canun ni pamoja na kuzuia uharibifu wa misitu kama moja ya njia ya kupunguza gesi zinazochafua mazingira.