Mabilioni ya watu bado wameachwa nyuma katika jamii ya kidigital:PGA

4 Septemba 2013

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amesema hivi sasa 1/5 ya nyumba zote katika mataifa yanayoendelea zimeunganishwa na mtandao wa internet hii ikiwa ni ongezeko la asilimia 13 ikilinganishwa na miaka mitatu iliyopita. Bwana Vuk Jeremic ameyasema hayo jumatano kwenye mjadala maalumu kuhusu uboreshaji wa kunganishwa na mtandao Eurasia. Hata hivyo amesema ingawa haya ni mafanikio makubwa lakini bado hatua kubwa zinahitajika ili kuziba pengo la kidigital baina ya mataifa ynayoendelea nay ale ynayoendelea.

(SAUTI YA VUK JEREMIC)

Ameongeza kuwa katika nchi tajiri asilimia 78 ya nyumba zimeunganishwa na mtandao wa internet na nyingi kwa kutumia mitandao ya gharama nadfuu na inayoaminika. Hii inamaanisha bado mabilioni ya watu hawana fursa ya kupata taarifa na kubadilishana elimu ambayo itawasaidia kuboresha maisha yao, bado hawajaunganishwa katika jamii ya kidigital ya karne ya 21.